Juhudi Za Kumaliza Ukeketaji Kwa Mtoto Wa Kike Zaendelezwa Pokot Magharibi
Wanaharakati mbalimbali wamekongamana na serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi katika wadi ya Alale kusisisitiza kujitolea kwao kukomesha ukeketaji ya wasichana katika eneo hilo.
Ikumbukwe tarehe sita mwezi Februari, dunia nzima iliadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, ikilenga kumaliza ukeketaji kwenye malengo lengwa ya ruwaza ya mwaka wa 2030.
Waziri wa Utamaduni, Utalii, Michezo na Vijana katika kaunti Pokot Magharibi Lucky Litole wameungana na washikadau kutoka Uganda katoa usaidizi kwa manusura,manghariba pamoja na watoto ambao wamekosa kupelekwa shuleni na wazazi wao.
Bi. Litole alieleza kuwa imebainika kuwa kuna majasusi walitoroka mjini wa Uganda baada ya kufanya kitendo cha ukeketaji na akasema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao watakaopatikana.
‘Tumefahamishwa kwamba kuna manghariba ambao bado wanaendeleza kitendo cha ukeketaji na baada ya kutekeleza wanatorokea mjini Uganda ili wasifikiwe na mkono mrefu wa sharia,’ Litole alisema.
Aidha ali
sema pia kuwa serikali ya kaunti Pokot Magharibi ina mpango wa kuanzisha vitua vya uokozi katika maeneo amabayo ukeketaji bado unashuhudiwa ili kuokoa watoto amabao bado wana ari ya kuendelea na masomo.
Aliomba serikali kuu na zile za kaunti kutoa msaada wa chakula kwa vituo hivyo punde tu vinapoanza kazi.
‘Kile tu ningependa kuomba serikali kuu na ile ya kaunti ni kwamba watusaidie katika kutusambazia msaada wa chakula vituo hivyo vikianza kufanya kazi,’ Litole alisistiza.
Bi Litole aliwashukuru wadau nchini Uganda na kuwahakikishia kuwa vyombo vya sheria vina mipango ya kukabiliana na wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji.
Kwa upande wake Mkururgenzi wa Wizara ya Watoto, Philip Opopa,alisema ana imani kuwa wageni kutoka nchi jirani watashirikiana kuhakikisha watoto wa pande zote wanapata huduma bora.
Aidha Opopa amelaani kitendo cha ukeketaji na kuozwa kwa mapema akisema kwamba ni utwelekezaji wa haki za mtoto msichana.
‘Mtoto msichana anapokeketwa na kuozwa mapema unampelekea kuathirika kiafya kwa
sababu mwili wake haujakuwa sawa wa kuweza kuwa mama,’ Opopa alieleza.
Tom Masinde, Meneja wa Programu katika World Vision, alisema viongozi wa Kenya na Uganda pamoja na watendaji ulinzi wa watoto wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa manufaa mabubwa kulinda watoto mpakani.
Masinde alisema hiyo inatokana na kwamba watu wanaoishi Kenya na Uganda wanakabiliwa na tatizo amabalo linawaathiri kwa njia moja au nyingine, mojwapo ni ukeketaji na huku wakilazimika kuingilia kati kuona jinsi ya kulikomesha janga hilo.
‘Jinsi tunavyoweza kushirikisha jamii, jinsi tunavyoweza kushirikisha kile ambacho tayari kinafanya kazi nchini Uganda na pia Kenya,’ alisema Masinde.
Alisema kuwa wataimarisha utekelezaji wa sheria, kuimarisha mawasiliano kuhusu masuala ua usalama, na kuwakamata wahalifu wanaojaribu kutoroka baada ya kufanya uhalifu.
Pia walizindua kampeni ya kurudi shuleni ili watoto wote wapate fursa sawa ya kwenda shule na kuwaweka salama.
Hata hivyo wadau hao walisema Ipo haja ya kushirirkisha wazee wa kimila ili
wawe kama kielelezo kwa lengo la kufikia kipengele cha kuwashirikisha manusura kama mabingwa kwani wanapozungumza na jamii wanazungumza kutokana na uweledi wao wa uzoefu.
‘Tuna pia mikakati ya jinsi tunavyoweza kuwashirikisha wazee wa kimila kwa sababu wazee ndio wasimamizi wa tamaduni na pia kuwashirikisha walionusurika kwa sababu jamii itawasikia vyema,’ alisema Masinde.
Source: Kenya News Agency